Pages

Subscribe:

ContactMe

Wednesday, September 4, 2013

Saturday, August 31, 2013

NEEMA YA PEKEE KWENYE KONGAMANO LA VIJANA WA MAKANISA YA IPHC TZ KANDA YA MASHARIKI.

TAZAMA KILE MUNGU ANAFANYA KWA WATOTO WAKE.
HAKIKA EBENEZER YU HAI.

KARIBU TUABUDU PAMOJA;
TUPO TABATA SEGEREA, DSM.

SIMU: 0757 007 150

Sunday, August 25, 2013

KONGAMANO LA VIJANA IPHC-KANDA YA MASHARIKI LAVUNJA REKODI. ''VIJANA NI NGUZO YA KANISA''

Zaidi Ya Vijana 70 Walihudhuria Kongamano Hilo.

Kongamano lilianza kwa uchaguzi huru wa viongozi wa vijana ambao ni:
1> Mwenyekiti wa vijana kanda ya mashariki/Dar es Salaam na wilaya.
2> Katibu wa vijana kanda ya mashariki na wilaya.
3> Mwekahazina wa vijana kanda ya mashariki.

Walengwa walikuwa ni viongozi wa vijana wa makanisa.

MATOKEO YA UCHAGUZI:
* Mwenyekiti aliyechaguliwa ni ''BARAKA KUMWENDA'' kutoka Kanisa La Ebenezer.
* Katibu aliyechaguliwa ni '' VASCO STEVEN'' kutoka Kanisa La Ebenezer, Alizoa kura zote.
* Mweka hazina aliyechaguliwa ni ''Elizabeth Shilla '' kutoka Kanisa La Kipunguni.

Vasco Steven (kushoto)_Katibu

Baraka Kumwenda_Mwenyekiti

Elizabeth Shilla_Mweka hazina
Mkurugenzi wa Vijana kanda ya Mashariki_ Mch. Shedrack Msogoye
Baada Ya Uchaguzi Kuisha, Mchungaji wa Ebenezer Magreth Marton Alihubiri:
Somo: Lijue Jina Lako
2Kings 2:1ff

Mch. Magreth Marton
Mchungaji Magreth alianza kwa mifano kama vile ilivyokuwa kwa Yesu Kristo wa Nazareth.
Ni habari ya mtoto asiyejua jina lake, ndipo baadae baba wa mtoto alipomwambia wewe unaitwa fulani.
Tokea hapo mtoto akajua jina lake na akaanza kuambatana na baba yake.

Hapa kuna watu/vijana ambao hawajui majina yao, lakini siku ya leo wamejua majina yao.
Ukilijua jina lako hutachoka kamwe kama ilivyokuwa kwa Elisha. Aling'ang'ana mpaka Eliya akamwambia omba lolote, akasema nataka ''sehemu ya roho yako''.

Sifa tatu za watu waliobadilishwa ( Transformed ) 
1. Lazima uamini mahali ulipo
_ ni lazima uheshimu viongozi
_ ni lazima ujiamini
 Elisha kwa kujiamini na kuamini mahali (position) alipo, akawaambia ''Ninajua, nyamazeni kimya''

2.  Lazima ubadilishwe (be transformed)
_ Elisha hakuishi kwa kanuni za wanadamu bali za Mungu baada ya kuwa transformed.

3. Lazima uwe na mtu nyuma yako (Mentor)

Kwa hakika Ibada Ilikuwa njema sana sana sana!
 




















 
 Mwisho tunasema;
Injili Mbele Yesu Juu!

+255 757 007 150 
Mch. Magreth Marton
 

 



Sunday, July 21, 2013

SUNDAY SERVICE _ Ebenezer IPH Church. Part 1.

Ibada ndani ya Kanisa la Ebenezer, Tabata Segerea!

Baraka akizungumza Neno la sadaka asubuhi ya leo!
Mch. Bachuba










jhg

Friday, July 19, 2013

OBI, MBWA 'MTUMISHI' ALIYEBADILI MAISHA YA JAMII KUMFUATA YESU


Hakika ni ajabu ukisikia, na hata ukiona ndio utashangaa zaidi – utashangaa kuona kuwa hata mbwa anatumiak kuvuta watu kanisani, na kuwapa faraja katika Kristo Yesu, na hatimaye kujifunza zaidi kuhusu Mwokozi Yesu na kumpokea. Ndivyo ilivyo kwa kanisa la Kreutz Creek Presbyterian lililopo Pennsylvania nchini Marekani lilivyojaliwa Neema ya pekee.


Mchungaji Marion Haynes-Weller anaeleza namna ambavyo mambo yalikuwa wakati wa mahojiano na Christian Post, “Tulikujua kwamba tuna kuna watoto kwenye hii mitaa yetu, na tulikuwa tukiwaona na kuwapungia mkono, lakini wengi wao sio watu wa kanisa – yaani wamejitenga na kanisa, hivyo inakuwa tabu unapoanza kumfuata kwa lengo la kumhubiria, na hawakuwa wanapenda”
Kanisa hilo ambalo lipo kwenye mji wenye takriban watu elfu sita, Hellam, York, sasa linabadili historia ya mji huo kutokana na namna ambavyo mitaa inabadilishwa kiimani, kutokana na Obi, mbwa ambaye amekuwa kivutio kwa watoto na wakazi wa jamii hiyo.
 
“NIlianza kuja naye kipindi akiwa mdogo hapa kanisani, hapo watoto walianza kukaa na kucheza nae.
Baada ya hapo nikawa namleta karibu kila Jumamosi kwenye ibada yetu ya usiku, lakini bado alikuwa mdogo sana kwahiyo watu wakawa pia wanakuja kumuona” Anaeleza mchungaji Haynes namna ambavyo mbwa huyo aliingia kwenye huduma yake. 
 
Kadri Obi alizidi kukua, ndivyo ambavyo alianza kuona tofauti ya mwenendo wake kwa watu ambao aliwavutia kuja kanisani.
Mch. Haynes, ambaye mume wake ni mwanasaikolojia mwenye paka anayefanya kazi ofisini kwao alikuwa pia hamasa kwake na kupelekea kugundua faida ya kuwa na mbwa huyo kwenye maeneo ya kazi yake ya utumishi, kwa kuwa anaweza kuwafanya watu wenye wakati mgumu angalau kupumua, nah ii sio kwa watoto tu, bali hata watu wazima.
Unajua watoto wakiwa kama wanataka kujakukaangalia ka-mbwa, mimi huwa nawaambia eeh karibuni mbwa yupo, basi mwanzoni ilikuwa ni watoto wachache, lakini sasa hivi imehamasisha watoto wa mtaa wote mara tu walipojua kuhusu taarifa hizi.
 
 Darasa likiendelea, mchungaji Haynes akiwa na Obi kwenye mafundisho picha kupitia Screen Grab via Daily Record/Sunday News


Mtazamo wa kanisa hili hivisasa umebadilika, yaani kutoka sifuri hadi kaya zaidi ya 20 ambazo sasa wankuja kanisani. Na si kwa watoto tu, hata walewatu wazima wasio na watoto nao huja kujumuika kwa pamoja na mbwa wao, jambo ambalo limeongeza idadi ya washiriki kanisani hapo, ambao kidogokidogo huubiriwa injili, ijapokuwa hawakuwa wanakuja kanisani mwanzoni.
Lakini katika hatua nyingine, Obi ameonekana msaada kwa watoto wasiojua lugha ya Kiingereza, ama kwa wale ambao kwao ni lugha ya pili. Kwani wasipokuwa na mtu wa kuongea, Obi anaweza kuzungumza nao, wanazungumza “dog language”
, ambayo karibu kila mtoto anaielewa.
Kanisa hilo kwa hivi sasa linaendesha mafunzo katika kipindi cha likizo, ‘Vacation Bible School Obi’, ambapo watoto wenye umri wa kuanzia miaka 6-14 wamepata fursa ya kuhubiriwa kuhusu Yesu, ambpo hapo awali hawakujua A wala B kuhusu hadithi za Biblia.
“Siku moja tulikuwa nje tunacheza na mbwa, na nikasema – unajua tunaweza kukaa na kupanga mikakati, nitawapa chakula na tutakuwa na maombi” Anaeleza Mchungaji Haynes na kasha mtoto mmoja akamuuliza, “maombi ni nini?” Akajibu “ni pale unapozungumza na Mungu”. Kisha mtoto mwingine akauliza, Mungu ni nani?
“Kuanzia hapo tukaanza sifuri, na hivi sasa watoto wanakuja na kuomba, na kufahamu hadithi za Biblia, kwa kuwa hawaijui kwani kuna siku walikuw wanaigiza kuhusu Musa, na hakuna akati yahao watoto aliyekuwa anmjua Musa ni nani, wengi walishamsikia Yesu, lakini Musa hakuwa akilini mwao.” Mchungaji Haynes anasema na kumalizia kwa kicheko kwamba, “Yaani saivi wanaombeana wenyewe kwa wenyewe na pia wanaombewa. Ni jambo jema kuona Mungu anatenda kupitia vitendea kazi tulivyo navyo, na muda huu kitendea kazi ni 80lb Labrador (aina ya mbwa).
Hakika ya Mungu ni mengi, chochote kinaweza kutumika kumhamasisha mtu kufika kanisani, ama kwenye kusanyiko lenye injili kuhubiriwa, na basi kwa mahali ulipo pia, unaweza kutazamia ni kitu gani kinaweza kuwapa hamasa watu kufika – ili wapata kumjua Yesu Kristo. Na katika yote,m tufanye kwa imani.
 
CHANZO: gospelkitaa.blogspot.com

Saturday, July 13, 2013

ZIFAHAMU TABIA ZA WANAUME WENYE MAPENZI YA KISANII "Players" (Usipozijua ni rahisi kukamatika)

Ili kukusaidia nataka kukupa tabia chache za wanaume wenye mapenzi ya kisanii. Kutokana na uzoefu ninaoupata katika kushuhulikia matatizo ya watu ya mahusiano na saikolojia, nimegundua kuwa wengi wanaolengwa na athari za tabia hizi ni wale wanaoingia au walioko katika mahusiano na wanaume wenye ndoa zao.

Tabia ya kwanza:

Daima ni watu wanaoepuka sana kutoa au hata kupokea zawadi, niwajanja sana katika hali ambayo wanakushawishi kujua kwamba hivi ndivyo walivyoumbwa, kwamba wako tayari kufanya mambo makubwa ya kimapenzi lakini sio vizawadi lakini ukweli ni kwamba wanaepusha mazingira ambayo yaweza kufanya washtukiwe na wake zao au mpenzi mwingine wa pembeni. Unajua katika zawadi mengi yaweza kutokea, wengine wamekamatwa na risiti za vitu walivyonunua, wengine wameulizwa hilo shati ulinunua lini? au hayo manukato mbona siyajui, yametoka wapi? Kwahiyo kuwa macho sana unapoona ishara hii kwa mpenzi wako.


Chris Mauki.

Inaendelea
Endelea kufuatilia blog hii, kwa mambo mengi zaidi gonga hapa  click here


Monday, July 8, 2013

USIINGIE KWENYE MAHUSIANO MAPYA KABLA HUJAMALIZANA NA MAHUSIANO YA AWALI.


Wewe ni shahidi kuwa wengi wetu tunaingia kwenye mahusiano baada ya mahusiano ya awali kuvunjika. Jambo hili sio baya na wala sio la kushangaza kwasababu kila mtu anauhitaji wa kuitimiza kiu ya kupenda na kupendwa ambayo ni hitaji la kimsingi kabisa la kila mwanadamu, kwa wale walio soma “Maslow’s hirachy of needs” watanielewa zaidi hapa. Tatizo linakuja kwenye “tunaanzaje mahusiano haya mapya?” na “je tumemalizanaje na yale ya awali?” Usiwe mwepesi kusema ndiyo kumkubali mpenzi mpya au kufungua mlango kwa penzi jingine wakati lile la mwanzo haujaufunga mlango ukafungika. Wengi wamejikuta wana penzi pande mbili baada ya kuanza mahusiano na mtu mwingine wakidhani walishamalizana na yule wa kwanza, tena hawakuwa wazi hata kwa huyu mpenzi mpya kumtaarifu kwamba ninakukubali ila kuna mtu bado hatujang’oa mizizi ili na yeye ajiandae kwa chochote kitakachotokea kesho. Baadae unajikuta kwenye njia panda inayoumiza sana moyo na kuleta msongo wa mawazo “stress” tena kwa kujitakia tu. Una haraka ya kwenda wapi? Usitumie kuharakisha kuingia kwenye penzi jipya kama maji baridi yakupooza maumivu yako ya penzi la awali. Hakikisha umepona kwanza majeraha yako ya kwanza kisha ufanye maamuzi halisi na thabiti ya kuanza tena mahusiano mapya. Kamwe usihusiane kwa nia ya kupooza vidonda vya ndani maana vikisha poa utakuja kugundua halikuwa penzi bali ilikuwa ni huduma ya kwanza tu. Ingia kwenye penzi ukiwa na uhakika na fanya maamuzi thabiti ili uwe tayari kwa kila yanayotokea ndani ya penzi hilo. Kumbuka “We love in order to stay, we don’t love in order to leave”


Chris Mauki.

ZITAMBUE TABIA NNE ZA IMANI _ Rev. Meinrald Mtitu



Kama kawaida ya blog hii ya kanisa, jumapili hii mtumishi wa Mungu Rev. Meinrald Anthony Mtitu aliuwasha moto na watu wengi waliponywa kwa namna ya ajabu na pekee sana! Ibada ilipoisha watu hawakutaka kuondoka.

Rev. Meinrald Anthony Mtitu katika fundisho lake alifundisha na kuhubiri zaidi juu ya mambo manne kuhusu tabia za Imani.










MAMBO MANNE KUHUSU IMANI:
Mwanzo 6:9--  
Kielelezo ni Nuhu.

1* Imani inamtumaini Mungu hata pale ambapo hapaleti maana yeyote, pale ambapo mazingira yanakataa lakini imani bado inatumaini wakati mtu mwingine akiangalia anaona huku ni kuchanganyikiwa.

Imani inatumaini mahali ambapo katika akili (reasoning) huoni maana - mahali ambapo hesabu zinakataa, formula zinakataa, principle zinagoma, Lakini imani bado inatumaini.
Pale ambapo mazingira yanakataa, ushahidi (facts) unakataa, lakini imani inasema ndio - na hii ndio tabia ya imani.

Kwa imani Nuhu akajenga safina.
Ikumbukwe kuwaNuhu hakuwahi kuona safina hapo kabla, lakini Mungu anamuambia utajenga safina. Pia Nuhu hajawahi kusomea kazi ya kutengeneza safina wala hakuwa engineer.

Hivyo imani inaamini wakati kila kitu hakileti maana. Bali italeta maana utakapotii na kuchukua hatua.

2* Imani haisubiri kuona, kugusa, kuhisi, kunusa au kusikia.
Nuhu alikuwa hajawahi kuona mvua lakini aliamini, maana tangu kuumbwa ulimwengu mvua ya kwanza kunyesha ilikuwa ni wakati wa gharika.
Nuhu alimuamini Mungu kwa kutarajia kuona kile Mungu alichokusudia kufanya.
Nuhu hakujua gharika itakuwaje, lakini alimwamini Mungu.

3* Imani inasubiri haikati tamaa.
Imani ni uwezo wa kusubiri ahadi ya Mungu juu ya neno fulani alilosema bila kukata tamaa.
Ibrahimu anaitwa baba wa imani kwa sababu alisubiri zaidi ya miaka 20 kupata mtoto.
Nuhu alisubiri miaka 120 ndipo mvua ikanyesha.

4* Imani inatii kile Mungu alichosema au kuagiza bila kujali kitakuwa kigumu kiasi gani, au kitakuwa na changamoto kiasi gani. Ndio maana inajengwa kwenye msingi wa neno la Mungu. Neno hili laweza kuwa la jumla (Logos) au maalumu ( Rhema ).

MUNGU AKUBARIKI.