Pages

Subscribe:

ContactMe

Monday, July 8, 2013

USIINGIE KWENYE MAHUSIANO MAPYA KABLA HUJAMALIZANA NA MAHUSIANO YA AWALI.


Wewe ni shahidi kuwa wengi wetu tunaingia kwenye mahusiano baada ya mahusiano ya awali kuvunjika. Jambo hili sio baya na wala sio la kushangaza kwasababu kila mtu anauhitaji wa kuitimiza kiu ya kupenda na kupendwa ambayo ni hitaji la kimsingi kabisa la kila mwanadamu, kwa wale walio soma “Maslow’s hirachy of needs” watanielewa zaidi hapa. Tatizo linakuja kwenye “tunaanzaje mahusiano haya mapya?” na “je tumemalizanaje na yale ya awali?” Usiwe mwepesi kusema ndiyo kumkubali mpenzi mpya au kufungua mlango kwa penzi jingine wakati lile la mwanzo haujaufunga mlango ukafungika. Wengi wamejikuta wana penzi pande mbili baada ya kuanza mahusiano na mtu mwingine wakidhani walishamalizana na yule wa kwanza, tena hawakuwa wazi hata kwa huyu mpenzi mpya kumtaarifu kwamba ninakukubali ila kuna mtu bado hatujang’oa mizizi ili na yeye ajiandae kwa chochote kitakachotokea kesho. Baadae unajikuta kwenye njia panda inayoumiza sana moyo na kuleta msongo wa mawazo “stress” tena kwa kujitakia tu. Una haraka ya kwenda wapi? Usitumie kuharakisha kuingia kwenye penzi jipya kama maji baridi yakupooza maumivu yako ya penzi la awali. Hakikisha umepona kwanza majeraha yako ya kwanza kisha ufanye maamuzi halisi na thabiti ya kuanza tena mahusiano mapya. Kamwe usihusiane kwa nia ya kupooza vidonda vya ndani maana vikisha poa utakuja kugundua halikuwa penzi bali ilikuwa ni huduma ya kwanza tu. Ingia kwenye penzi ukiwa na uhakika na fanya maamuzi thabiti ili uwe tayari kwa kila yanayotokea ndani ya penzi hilo. Kumbuka “We love in order to stay, we don’t love in order to leave”


Chris Mauki.

0 comments:

Post a Comment